Gishubi (Gitega): Mzee wa miaka 60 alipatikana amekufa nyumbani kwake

SOS Media Burundi
Gitega, Agosti 28, 2025 – Mwili wa Emmanuel Nyandwi, mwenye umri wa miaka 60, ulipatikana Jumatano, Agosti 27, 2025, ndani ya nyumba yake kwenye kilima cha Nyamutobo, wilaya ya Nyabiraba, tarafa ya Gishubi, katika mkoa wa Gitega, katikati mwa Burundi.
Polisi wanaripoti kuwa hali halisi ya kifo hicho bado haijajulikana na uchunguzi unaendelea. Kujiua kwa sasa kunazingatiwa, kwani mwathiriwa alikuwa peke yake nyumbani wakati wa mkasa huo. Hakuna washukiwa wametambuliwa.
Ugunduzi huu unakuja siku chache baada ya Agosti 23, 2025, wakati mwili wa Mathias Mpfekurera, 69, ulipopatikana katika Mto Ruvyironza, kwenye kingo za kilima cha Jurwe, katika tarafa hio ya Gishubi.
Matukio haya ya mara kwa mara yanazua wasiwasi miongoni mwa wakazi. Mamlaka za mitaa zimehimiza tahadhari na kuhakikishia kwamba hatua zote muhimu zitachukuliwa kuchunguza kesi hizi na kuzuia hali kama hizo kutokea tena.
Waangalizi wengi sasa wanataja mkoa wa Gitega kama « mkoa wa makaburi » kutokana na kupatikana mara kwa mara kwa maiti katika eneo hilo.