Bururi: watu wawili waliokamatwa kwa kukataa kusajiliwa

Arcade Nzisabira, umri wa miaka 32, na Jacqueline Nibizi (umri wa miaka 40) kutoka kilima cha Burunga katika eneo la Gasanda, katika wilaya na mkoa wa Bururi (kusini mwa nchi) wamezuiliwa katika seli za polisi huko Bururi tangu Jumapili hii. Wanashitakiwa kwa « kukataa kuhesabiwa ».
HABARI SOS Media Burundi
Maafisa wa eneo hilo walisema watu hao wawili walikataa kusajiliwa kama sehemu ya sensa inayoendelea nchini Burundi.
Katika mikoa kadhaa, wafuasi wa madhehebu tofauti walisitasita kujibu maswali kutoka kwa wachukuaji wa sensa wakimaanisha « vitendo vya kishetani. » Katika visa vingi, utawala wa eneo uliwalazimisha kujiandikisha.
Tangu Agosti 16, sensa ya watu, makazi, kilimo na mifugo imekuwa ikifanyika katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki.
Sensa hii, ambayo inapaswa kufungwa Jumapili hii, imeongezwa kwa siku tano, alitangaza jumapili Nicolas Ndayishimiye, rais wa Ofisi Kuu inayohusika na sensa (BCR). Alieleza kuwa kiwango cha kuorodheshwa kilichopatikana tayari ni 98.4%. Mkoa uliyoshika nafasi ya kwanza ni Buhumuza kwa ushiriki wa asilimia 99.7, ile ya Bujumbura ikiwa katika nafasi ya mwisho kwa asilimia 96.3.
———
Kituo cha sensa nchini Burundi