Derniers articles

Rumonge: Kanda 4 zenye viongozi wapya

Leonard Sirabahenda aliteuliwa kuongoza kanda ya Kizuka, Michael Ntahondo sasa ndiye mkuu mpya wa kanda ya Minago wakati Innocent Nijimbere aliteuliwa kuongoza kanda ya Kigwena. Hamza Sinankwanabose sasa ndiye mkuu mpya wa kanda ya mji wa Rumonge. Haya ni maeneo ya wilaya na mkoa wa Rumonge (kusini-magharibi mwa Burundi).

HABARI SOS Media Burundi

Wakuu wa zamani wa kanda za Kizuka, Minago na Kigwena walibadilishwa Juni 18, 2024 kwa « sababu za uzembe », kulingana na chanzo cha utawala.

Aliyeongoza kanda ya Rumonge alibadilishwa kwa kuteuliwa kufanya kazi nyingine.

Baadhi ya wakazi wa Rumonge wanaona uteuzi wa sura hizo mpya kama marekebisho ya chama tawala kujiandaa na uchaguzi ujao wa wabunge mwaka 2025.

Machifu wapya 4 wa kanda ni wanachama wa chama cha CNDD-FDD, kama wakuu wa kanda wanaoondoka.

———-

Barabara katika mji wa Rumonge (SOS Médias Burundi)